Nilimpa shavu kujipima ubavu!
Ikiwa ina muda c mrefu sana lakini bado ikiwa inafanya vizuri kwenye vituo vya television vya nyumbani na hata vya nje ikiwemo Channel O,wimbo 'ZERO' wa mwanadada Witness... akiwa amemshirikisha mzee wa kazi FID Q..amesema ameutoa kwa nia ya kujipima nguvu.
Akielezea kuhusu kumshirikisha mbaya huyo wa miondoko ya Hiphop..yaani Farid Kubanda 'FID Q' anasema: “Nimeamua kumshirikisha Fid Q kwenye wimbo huo kwa sababu namuamini ni msanii wa kiukweli, hivyo niliamua kumshirikisha ili nijipime ubavu nione kama angenifunika.
“Fid Q amekuwa na sifa ya kuwafunika wasanii wengi wanaoshirikiana naye katika kufanya kazi lakini kwangu imekuwa tofauti, kwa pale naweza kusema ilikuwa ngoma droo kwa hiyo nilijiona mi mkali.”
Witness anasema kwamba mwaka huu ameachia albamu yake ya nyimbo 10 inayojulikana kama ‘Khaya! Khaya! Khaya!’ ikiwa inamaanisha (aya!, aya!), ikiwa na vibao kama ‘Khaya! Khaya! Khaya!’ yenyewe iliyobeba jina la albamu, Usipime, Kichekesho, Salva, Witness na nyinginezo.
Kwa mujibu wa Witness, anasema kwamba albamu hiyo imeanza kuuzwa rasmi nchini Norway Aprili 8, mwaka huu kwenye mtandao wa I tune wa nchini Norway.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki
Print nakala