Nyamagana haibadilishwiiiii
Katika hali ambayo haikutegemewa na wengi kutokana na kauli za kujichanganya zinazotolewa na viongozi kadhaa kuhusu kubadilishwa kwa matumizi ya Uwanja wa Nyamaga,hatimaye Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika ameamua kulitolea uvivu swala hilo.
Mkuchika aliamua kuingilia swala hilo kwa kusema kuwa kitendo cha serikali kuwaomba madiwani kubadilisha uamuzi wao wa kubadili matumizi ya Uwanja wa Nyamagana ni heshima tu, lakini mpaka hivi sasa yeye kama waziri mwenye dhamana ya michezo anaelewa kuwa serikali haijakubaliana na kubadilishwa kwa uwanja huo.
Mwanzoni mwa wiki,Mkuchika alikaririwa akitoa maoni yake kama waziri anayehusika na michezo akiwaomba madiwani wa Nyamagana,wabadili uamuzi wao ili uwanja huo uendelee kutumika kwa ajili ya michezo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipotakiwa kutoa msimamo wa serikali Jumanne, alimtaka mwandishi aende kwa waziri anayehusika na michezo.
Ndipo, Mkuchika aliamua kulitolea uvivu suala hilo, ambalo limekuwa kero kwa wakazi wa Halmashauri ya Nyamagana.
"Tunaposema tunawaomba madiwani wabatilishe uamuzi wao, tunawapa heshima," alisema Waziri Mkuchika mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kuwapongeza wachezaji wa Taifa Stars kwa kuishinda Uganda iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa juzi usiku.
"Lakini hiyo haimaanishi kuwa wanaweza kujifanyia watakavyo. Uwanja wa Nyamagana utabakia kuwa wa michezo."

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala