Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Riadha kigugumizi kwa kocha wa kigeni

Kile Chama cha Riadha Tanzania (RT) kilisema baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema anataka kusaidia mchezo huo kwa kutafuta kocha wa kigeni, chama hicho kimesema hakitakurupuka mpaka wakusanye maoni ya wadau mbali mbali kuhusu nini cha kufanya.



Naye Katibu Mkuu wa RT Suleiman Nyambui alisema wao hawawezi kuipinga kauli ya Kikwete , bali wanachosubiri ni maoni kwa wadau wa mchezo huo.

Nyambui alisema jambo hilo ni la kitaifa na sio RT, kwanza lazima tukusanye maoni ya wadau wa mchezo na kisha yajadiliwe.

Alisema inawezekana tatizo ikawa si kocha, kwani kupitia maoni hayo tunaweza kupata kitu tofauti na mawazo ya kutafuta kocha.

Alisema kwa sasa kikubwa wanachofanya ni kukusanya maoni ya wadau, na kuyapeleka katika Kamati ya Ufundi.

Alisema baada ya kupitisha mapendekezo hayo ndipo watakutana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kwa mambo mengin



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.