Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Hasheem na mamilioni ya mbovu

Hii ni baada ya wanamichezo wawili wa Tanzania kuingia mikataba minono, itakayowaingizia mamilioni ya 'mbovu' shilingi.



Si mwingine bali ni chipukizi Hasheem Thabeet ambaye ni mchezaji mcheza wa mpira wa kikapu wa Tanzania, atakayechezea timu ya Memphis Grizzlies ndani ya msimu ujao wa ligi kuu ya kikapu nchini Marekani NBA.

Kwani Hasheem anatarajia kulamba mshahara mnono, wa dola dola za kimarekani milioni 14,379,840 (shilingi bilioni 19,125,187,200) kwa mwaka.

Dau hilo linamfanya nyota huyo wa NBA kuingiza kiasi cha shilingi bilioni 1,593,765,600 kwa mwezi na kuzidi kwa mbali kabisa kiungo wa Simba na Taifa Stars, Henry Joseph aliyesajiliwa nchini Norway na klabu ya Kongsvinger atayepokea dola 200,000 (Sh 260 milioni) kwa mwaka.

Hasheem alikuwa mchezaji wa pili kuchaguliwa kujiunga na NBA msimu ujao, kati ya mamia ya wachezaji wanaowania kupata nafasi ya kucheza katika ligi hiyo mashuhuri duniani.

Kwani Mchezaji aliyechaguliwa wa kwanza kujiunga na timu ya L.A Clippers anayeitwa Blake Griffin atakuwa akilipwa dola za kimarekani milioni 16,071,840 kwa mwaka.

Akifuatiwa na James Harden ambaye alikuwa mchezaji wa tatu kuchaguliwa kujiunga na NBA ambapo atachezea Oklahoma City atakuwa akilipwa dola za kimarekani milioni 12,913,440 kwa mwaka.

Huku wachezaji wengine wakiambulia vifuta machozi ni pamojana Tyreke Evans ambaye alikuwa wanne kuchaguliwa, na atajiunga na timu ya Sacramento atalipwa dola za kimarekani milioni 11,642,640 kwa mwaka.

Na mchezaji wa tano kuchaguliwa Ricky Rubio atakayejiunga na Minnesota atakuwa akilipwa dola milioni 10,542,960.

Hapo awali Hasheem alikuwa akisoma na kucheza kikapu katika chuo kikuu cha Marekani, ambapo aliwahi kuchaguliwa mara mbili mchezaji bora wa ulinzi ukanda wa mashariki wa Marekani.

Hasheem alikuwa katika kundi la wachezaji waliokuwa wanatarajia kujiunga na ligi kuu ya kikapu nchini Marekani.




 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.