Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Sasa kumekucha

Kwa sasa wako katika maandalizi kabambe, ya kujiandaa na Ligi hiyo inayotarajiwa kuwika mwishoni mwa mwezi huu hapa hapa kwenye jiji la Lukuvi.



Ni wale washiriki wa Ligi ya mchezo wa ngumi na mateke (kick boxing), naye Mratibu wa ligi hiyo si mwinge ni yule bingwa wa dunia Japhet Kaseba, alisema maandalizi ya ligi hiyo yamekamilika na huku ligi hiyo ikitarajia kuwika Februari 27.

Alisema anashukuru mpaka sasa kikosi chake kinaendelea na maandalizi mazuri ya kutaka kujiachia, kwani wachezaji hao wana ari kubwa na Ligi hiyo kwani wanategemea Ligi hiyo itakuwa na mvuto wa hali ya juu.

Kwani bingwa wa Ligi hiyo ataibuka siku hiyo na zawadi ya pikipiki kubwa ya kisasa, huku zawadi nyingine zitaanikwa hapo baadaye.

Kaseba alisema mikoa 10 imethibitisha kushiriki ligi hiyo, huku washiriki wake wameshawasili kambini.

Na mikoa itakayoshiriki siku hiyo ni pamoja na Kigoma, Mara, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Pwani pamoja na Dar es Salaam.




 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.